skip to Main Content
+255-716-581-629 v.pius.pv@gmail.com
Fursa Zilizopo Katika Biashara Ya Mtandao(Network Marketing)

Fursa Zilizopo katika Biashara ya Mtandao(Network Marketing)

Biashara ya Mtandao ni Nini?

Biashara ya Mtandao ni mfumo wa usambazaji wa bidhaa wa kampuni  husika kwenda kwa walaji wake kwa kupitia walaji wanachama kama mawakala.

Mfumo huu unahusisha kusajili watumiaji wa bidhaa kama wanachama katika kampuni na kisha watumiaji hao husambaza habari juu ya bidhaa hizo kwa wengine kuwashawishi wajiunge na kisha kununua bidhaa.

Kampuni husika huwalipa wasambazaji kamisheni kulingana na watu wanaojiunga na kununua bidhaa kupitia kwao.

Si kazi rahisi kumiliki kampuni au biashara,kuna changamoto nyingi zikiwemo mahitaji ya watu wa kuajiri ili kufanya kazi ,sehemu ya ofisi,sehemu ya kuhifadhi bidhaa kabla hazijasambazwa n.k lakini kupitia makampuni ya mtandao kila mmoja anaweza akaanza biashara kwa mtaji kidogo sana bila kuwa na wasiwasi ya gharama hizo kubwa za kuanzisha biashara binafsi kama katika biashara za kawaida.

Katika biashara ya mtandao unaweza kuanza na mtaji mdogo tu hata chini ya Tsh 50,000/=

Fursa nyingine ni kuwa utapata nafasi ya kukutana na kufanya kazi na watu wenye uzoefu tayari katika biashara ambao wako tayari kukufundisha na kuona kuwa unafanikiwa. Sababu nao wanafanikiwa pale wewe unapofanikiwa.

Katika biashara hii unatumia nguvu kidogo kupata matokeo makubwa kwasababu ya “Nguvu ya Wengi” – Yaani unawatafuta na kuwafundisha wachache ambao nao watafanya hivyo hivyo kwa wengine na hivyo kujenga mtandao mkubwa wa watu chini yako. Lakini ili kujenga timu ya awali utahitaji kufanya kazi kubwa mwanzoni.

Misingi ya Mafanikio Katika Biashara ya Mtandao

Kama ilivyo kwa biashara nyingine yoyote, biashara hii imejengwa kwa misingi hiyo hiyo. Zifuatayo ni misingi mikuu ya kufanikiwa katika biashara ya mtandao:

  1. Wekeza pakubwa ili kupata pakubwa, au wekeza kidogo ili kupata kidogo – Kiasi utakachowekeza katika fedha au muda wako kutatoa matokeo yanayowiana na nguvu zako
  2. Usikate Tamaa Mapema – Ukitaka kufanikiwa ni sharti uvumilie hadi mwisho na usiache, huwezi jua ,pengine pale unapoacha ulikuwa unakaribia mafanikio
  3. Jifunze Elimu ya Biashara – Fahamu namna ya kuwatafuta wateja,kuelezea bidhaa ya kampuni yako na kushawishi wajiunge (Kufunga mauzo). Haya yote utajifunza utakapoanza toka kwa wale wa juu yako,usihofu kama si mzuri bado.
  4. Jenga na Kuza Mtandao wa Watu– Biashara ya Mtandao ni kuhusu mahusiano,unatakiwa kujenga mtandao wa watu ambao wataona na watapenda kufanya unachokifanya.
  5. Uongozi Mzuri – Unatakiwa kuwa kiongozi mzuri unayeenda kwa vitendo. Watu wanapenda kujiunga kwa viongozi wazuri- ni asili yetu.
  6. Fundisha Mbinu za Mafanikio – Wafundishe walio chini yako kufanya kama unavyofanya ili nao wafanikiwe na wewe pia. Utatakiwa kuandaa semina za mafunzo na kuwaalika watu kusikia habari nzuri.
Back To Top