skip to Main Content
+255-716-581-629 v.pius.pv@gmail.com
Zijue Faida Za Tovuti Kwenye Biashara Yako.

Zijue faida za tovuti kwenye biashara yako.

1. Tovuti yako hupatikana mwaka mzima kwa siku 7 za wiki, saa 24.
Endapo utafungua tovuti, itakuwa wazi na itakuwa ikitoa taarifa muhimu kwa wateja wako saa 24 kwa siku, siku 7 za wiki kwa mwaka mzima. Tovuti hutoa taarifa kuhusu biashara yako hata pale unapokuwa umelala.

Ione tovuti yako kama afisa mauzo asiyelala, anayekesha saa 24 siku 7 za wiki kutoa taarifa muhimu kuhusu biashara yako; nini mnajishughulisha nacho, kazi zako za hivi karibuni, bidhaa zako pamoja na shuhuda za wateja wako. Si hayo peke yake; tovuti hukuwezesha kufanya mauzo pia.

2. Tovuti huwasaidia wateja kukupata kwa urahisi
Kadri siku zinavyokwenda ndio jinsi ambavyo imekuwa rahisi kwa watu kupata taarifa mikononi mwao. Uwepo wa simu za kisasa ambazo zinawawezesha watu kutumia chombo cha kutafutia vitu yaani search engine kutafuta vitu wanavyohitaji pale wanapohitaji.

Kwa wastani inasemekana kuwa katika sekunde moja watu elfu arobaini hufanya maulizo yao kwenye mtandao wa Google (source). Hiyo ni sawa na maulizo bilioni tatu na nusu kwa siku na trilioni 1.2 kwa mwaka!

3. Washindani wako wamekuzidi
Kama washindani wako wana tovuti basi watakuwa wana nafasi nzuri zaidi ya kujitangaza. Na wewe ingia kwenye ushindani kwa kuwa na tovuti yako.

4. Anuani za barua pepe hufanya kampuni yako iaminike zaidi
Tovuti huwa na nafasi za anuani za barua pepe ya biashara yako, kwa mfano mauzo@biasharayako.co.tz. Matumizi ya barua pepe za kibiashara kama hizi zitafanya kampuni yako iaminike zaidi.

5. Tovuti ni njia rahisi ya kutangaza biashara kuliko njia za kizamani
Je ushawahi kuweka tangazo kwenye magazeti au majarida? Hebu jaribu kulinganisha gharama za kutangaza na kwa haraka sana utatambua kuwa gharama za tovuti ni ndogo ukilinganisha na njia za kizamani za utangazaji. Na hata pale unapotangaza kupitia magazeti pamoja na njia zingine, anuani ya tovuti yako huwashawishi wateja kuangalia tovuti yako.

Je unafikiri unahitaji kuwa na tovuti? karibu nikuhudumie Bonyeza hapa

Back To Top