skip to Main Content
+255-716-581-629 v.pius.pv@gmail.com
Ijue Biashara Ambayo Ina Risk Ndogo Sana Ya Hasara Na Mtaji Mdogo Sana- Affiliate Marketing

Ijue Biashara ambayo ina risk ndogo sana ya hasara na mtaji mdogo sana- Affiliate marketing

Affiliate marketing ni biashara inayofanyika ku promote biashara fulani inunulike na inaponunulika wewe unapata commission kutoka kwa mmiliki huyo.

Biashara hii inachohitaji ni wewe kuwa mzuri wa kufanya promotion tu na kizuri zaidi huwa haihitaji uangaike kwa kutembea na jua kali au mvua kwasababu huwa mara nyingi inafanyika kupitia mtandao ni mara chache sana ndio inaweza kulazimu utembee kama biashara hiyo inahitaji ukutane moja kwa moja na mteja husika.

1.Mfano wa Affiliate marketing inayohitaji ukutane na mteja moja kwa moja ;ni kuuza line za simu za makampuni mbalimbali kama Airtel,Tigo, n.k

Makampuni ya simu huwa yanatoa commission kupitia mawakala wao wanaouza na kusajiri line zao hivyo biashara hii uleta faida kubwa kama idadi ya wateja waliosajiliwa ni kubwa.

2.Mfano wa Affiliate marketing isiyohitaji ukutane na mteja moja kwa moja;ni kuwa forward wateja kwenye website inayousika na uuzaji wa software husika au bidhaa fulani na endapo watanunua na wewe utapata commission,kinachohitajika hapa ni kujisajili kwenye website inayouza bidhaa na watakupatia link ambayo itatumika kwenye website yako,website ambayo ni kituo cha wateja kwenda kwenye website ya mauzo kupitia link uliyopatiwa wakati wa usajili.

Hitimisho:

Biashara hii ya Affiliate Marketing inafaida kubwa sana na risk ndogo kuliko Network Marketing sababu haitegemei pyramid level ambayo inahitaji level ya watu wengi na mtaji mkubwa pasipo matumaini ya kurudisha pesa yako na kupata faida.

Je umefikiria kufanya Affiliate marketing ya mfano wa pili na ukahitaji website karibu nikuhudimie kwa website bora inayoweza onekana vizuri kuanzia Simu,Laptop mpaka Desktop. Bonyeza hapa kuwasiliana nami

Back To Top